SwahiliEnglish
            Lost Password?    Click here to register
 

Results 211 - 240 of 2067
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amepiga marufuku uamuzi wa Manispaa ya Kinondoni kuuza kwa mfanyabiashara mmoja maarufu eneo la ufukwe la Coco Beach

CCM kimesema kwa sasa hakiwezi kuzungumzia kauli ya Mwenyekiti wa Taifa Mstaafu wa chama hicho, Benjamin Mkapa kwamba si tajiri kama watu wanavyodhani na kwamba anaishi kwa kutegemea pensheni ya Urais

Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, katika bajeti ya mwaka huu, matumizi ya kuiendesha serikali yatatokana na fedha zake bila kutegemea wafadhili  

MAASKOFU wa makanisa kadhaa kupitia kile wanachokiita Ushirika wa Maaskofu Tanzania, wameandika waraka maalumu wenye ujumbe mkali na mzito kwa serikali, wakitaka kuchukuliwa kwa hatua kubwa ili kulinusuru taifa

Rais Jakaya Kikwete ameteua majaji 11 wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania, huku 7 kati yao wakiwa wanawake. Taarifa iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi, Ikulu, Bw. Philemon Luhanjo ilisema uteuzi huo umeanza Mei 24 mwaka huu

Timu iliyoundwa na Raisi dhidi ya kufuatilia pesa zinazodaiwa kuchotwa Benki ya Tanzania BOT kupitia akaunti ya madeni ya nje EPA, ikiwa inaendelea na kazi yake, imekutana na kasheshe jingine jipyaa na safari hii likiwa linadaiwa kuwa baadhi ya fedha...

Msanii DePlaizer ameweka wazi kuhusiana na hisia zake za kutaka kufaya kazi na wanamuziki wa barani afrika ikiwa ni moja katika malengo yake katika kuunyanyua muziki wa kifrika duniani

Timu ya Soka ya Taifa, Taifa Stars jana ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Timu ya Taifa ya Malawi katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja mpya Dar es Salaam

Kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu wa madini wilayani Mahenge, inayowakabili maofisa 13 wa Polisi akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Abdallah Zombe inaanza kuunguruma leo

Baadhi ya wazee wa kabila la Wahehe wamekuja juu na kutoa siku 30 kwa yeyote aliyehusika kwa njia moja ama nyingine na kifo hicho, kujisalimisha kijijini Luganga, Mufindi mkoani Iringa alikozaliwa gavana huyo la sivyo wamedai patakuwa hapatoshi

HUKUMU ya mahakama kuruhusu watu kugombea nafasi za uongozi kama wagombea binafsi, imemsukuma Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, kuchukua hatua zaidi ili kuhakikisha Watanzania wanaifaidi haki hiyo ya kidemokrasia

SERIKALI imesema Watanzania wote waishio Afrika Kusini wako salama kufuatia vurugu zilizozuka nchini humo zilizotokana na wenyeji kuwashambulia na kuwaua wageni kutoka nchi zingine

Wana CCM waliopanguswa katika chaguzi zilizopita ndani ya chama hicho wakiwemo baadhi ya majeruhi wa 'ajali za kisiasa' zilizotokea hivi karibuni wanadaiwa kuanza mkakati wa kujiweka sawa na kujipanga upya ndani na nje ya chama hicho

SERIKALI imesema haihusiki na kifo cha aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), Dk. Daudi Ballali kama uvumi unaoendelea kuvumishwa na watu mbalimbali kuhusu kifo hicho  

Wataalamu wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) na wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), jana walikwama kutatua tatizo la ukosefu wa umeme visiwani hapa kutokana na kukosa vitendea kazi

Lady Jay Dee a.k.a Jide antarajia kutumbuiza katika sherehe yakuzaliwa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini mheshimiwa Nelson Mandela ambayo inatarajiwa kufanyika jijini London nchini Uingereza mwezi Juni tarehe 27 mwaka huu

Bingwa wa zamani wa ndondi katika uzito wa juu duniani, Iron Mike Tyson, anatarajiwa kutua nchini Septemba mwaka huu akiambatana na bondia Laila Ali, ambaye ni binti wa nguli wa masumbwi duniani, Muhammed Ali

JESHI la Polisi nchini limefanya mabadiliko makubwa ya kuwastaafisha kazi askari wake kwa mujibu wa sheria, huku wengine wakibadilishwa vituo vya kazi  

Serikali ya Brazil imesema ina nia ya kuleta nchini teknolojia ya kutengeneza mafuta ya mabaki ya miwa yanayoweza kutumika kama mbadala wa petroli. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana

Asilimia 93 ya Watanzania hawajaambukizwa virusi vya ukimwi na kwamba jitihada zaidi zinaelekezwa katika kuwajali asilimia saba ya wale ambao tayari wameshaambukizwa virusi hivyo ili waweze kupata huduma zinazostahili

Baadhi ya wakazi jijini Dar es Salaam wameitaka serikali iwapatie ulinzi dada zake na aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania BOT

Watanzania wanaoishi nchini Afrika Kusini, wamekimbilia kituo cha polisi cha Jeppe, jijini Johannesburg na sasa wameiomba serikali ya Tanzania iwasaidie waweze kurejea nchini.

Aliyekuwa gavana wa Benki Kuu ya Tanzania(BOT) Daudi Balali amefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita huko nyumbani kwake, Washington DC, nchini Marekani

Mwanamitindo maarufu hapa nchini almaarufu kwa jina la Ally Rehmtullah hivi karibuni anatarajia kuzindua mavazi yake ambayo yanatarajia kujulikana kwa jina la Sex In The Event, linalotarajiwa kufanyika katika hotel ya Kilimanjaro Kempinski

Chama cha Wananchi (CUF) kimejibu kauli iliyotolewa na Rais Aman Abeid Karume wa Zanzibar ya kuwapa sharti viongozi wa chama hicho kabla ya kukutana kwenye mazungumzo ya kuleta muafaka wa kisiasa visiwani humo

Raisi wa Zanzibar Amani Abeid Karume, ametoa masharti ya kukutana na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, kuhusu Muafaka na kumtaka kwanza amtambue kuwa ni Rais halali aliyechaguliwa kwa kura nyingi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Abas Kandoro, amestushwa na "usanii" wa mikataba ya ujenzi wa barabara kadhaa za manispaa za Jiji lake na kueleza kuwa kuanzia sasa ataripoti kwenye Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini

Kundi la watu wasiozidi 15 wanaotuhumiwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha za kivita, wamevamia basi moja la abiria kulilipua kwa mabomu na na kusababisha vifo vya watu wawili papo hapo

WATU saba wamekufa papo hapo na wengine 11 kujeruhiwa katika ajali mbaya ya basi dogo aina ya Toyota Hiace ‘kipanya’, lililokuwa likisafiri kutoka Tukuyu mjini, Wilaya ya Rungwe kuelekea Kyela

Mtafaruku mkubwa uliibuka juzi katika hoteli ya Bwawani, visiwani Zanzibar baada ya baadhi ya viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) na NLD kutaka kutwangana wakati wa kikao

  

Powered by AlphaContent Bongo5.com © 2005-2008 - All rights reserved
Total Members
total 20276 registered
female 5045 female
male 15149 male
month 273 new this month
New: mkapa
Who's Online Now
We have 13 guests online and 2 members online
Bongo carlz
Bongo5 Chat Zone 2.0
Total of members in the chatroom:
2006-2007 © Copyright Bongo5.com