Burudani

Collabo ya Ommy Dimpoz na TID inakuja!

Ommy Dimpoz anatarajia kufanya ngoma na aliyewahi kuwa bosi wake wa takriban miaka minne, Khalid Mohamed aka TID kupitia Top Band. Taarifa hiyo inavunja tetesi zilizowahi kuandikwa kuwa wawili hao hawana uhusiano mzuri.

1422391_10151785278848379_1578152503_n

Akizungumza na Global TV, Ommy amesema ataendelea kumshukuru TID kwakuwa ndiye aliyempa nafasi ya kuonesha kipaji chake.

“Sasa hivi tuna ratiba ya kutoa nyimbo, so si unajua namshukuru kwa sababu alinipa nafasi,” alisema hitmaker huyo wa Tupogo.

“Unajua katika maisha, kila kitu kina chanzo, kwaHiyo ni lazima ushukuru. Siku zote katika mwanzo usi-focus kwenye hela zaidi, focus kwenye kujifunza kwahiyo nimejifunza vitu vingi kutoka kwake. Kwa band watu wote tuliokuwa kwenye band kwa sababu mnajua band mnakuwa watu wengi, kupitia kwake watu wengi nilijuana nao na ndo watu hao waliokuja kunisaidia.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents