Burudani
Collabo ya Beyonce na Rihanna yanukia?
Rihanna na Beyonce huenda wakaachia wimbo wa pamoja hivi karibuni.
Mtandao wa Digital Spy umedai kuwa wasilisho kwenye mamlaka ya ASCAP (database ya wasanii watumbuizaji ambapo wasanii na waandishi wa nyimbo wanatakiwa kuwasilisha nyimbo zao nchini Marekani) inaonesha kuwasilishwa wimbo “Blow” wa Beyonce na Rihanna.
Beyonce na Rihanna hawana uhusiano mzuri kutokana na tetesi kuwa Jay Z amewahi kuwa na uhusiano na Riri.