Events

Coca Cola kuwashusha wasanii Coco beach na helicopter?

Tangu kutolewa matangazo ya shoo ya kampuni ya vinywaji baridi Coca cola kuhusiana na shoo yao ya “Zeroed”, kumekuwa na speculation zinazozunguka kwa wanajamii juu ya mlio wa helicopter ambao unasikika katika matangazo ya radio ukihabarisha kuhusiana na shoo hiyo inayotarajiwa kufanyika siku ya Jumapili hii katika viwanja vya fukwe za coco beach.

page

Jambo moja kubwa ambalo limekuwa linazungumziwa sana ni usiri wa maana kamili au dhumuni la shoo hiyo ya Zeroed huku duru za kimbea zikibashiri surprise ya wasanii kuletwa Coco Beach na Helicopter.

Shoo hiyo inatarajiwa kufanyika kuanzia majira ya saa sita mchana na wasanii Linah, Joh Makini, Wanaume TMK, Dj Zero, Ommy Dimpoz na Swat Team wanatarajiwa kutoa burudani.

Haya sasa tunasubiri kuona nini hasa kitatokea na kukuhabarisha mdau wetu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents