Siasa

CNN yamhoji Rais Kikwete kuhusiana na mauaji ya tembo na Ushoga, tazama video hapa

“Wakati wa uhuru Tanzania ilikuwa na 350,000 .. mwaka 1987 kulikuwa na tembo 55,000 waliosalia.” Hayo ni maneno ya Rais Jakaya Kikwete aliyezungumza na mtangazaji wa CNN, Christiane Amanpour kuhusu namna Tanzania inavyopambana na uwindaji haramu.

Rais Kikwete alihojiwa na Amanpour jijini London, ambako wakuu wa nchi wanakutana kutafuta suluhisho la uwindaji haramu kabla hawajachelewa. “Huu ni wehu sasa, haiwezekani kabisa.. ni jambo kubwa.”

Mtangazaji huyo pia alimuuliza kuhusiana na suala la haki za mashoga barani Africa na ambapo Kikwete alisema itachukua muda kwa watu wa Afrika kukubali masuala ambayo nchi za Magharibi zinakubali. Na alipoulizwa kama angetaka kuona hilo linatokea, Rais Kikwete Amanpour “Siwezi kusema hilo kwa sasa”.

Tazama mahojiano hayo hapo juu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents