Habari

Club Bilz: ‘Tulifanya marekebisho ili kuwa club namba moja Afrika’, ifahamu ratiba ya wiki

Club Bilicanas imefanyiwa marekebisho makubwa na kuifanya si tu kuwa na jina jipya ‘Club Bilz’ bali pia club ya kisasa zaidi kuliko zote nchini.

IMG-20150129-WA0008

Kwa mujibu wa mkuu wa kitengo cha burudani wa Club Bilz au Bilz Night Club, Raheem Da Prince, matengenezo hayo yalilenga kuifanya Bilz kuwa club namba moja Afrika.

“Investiment ambayo imefanyika ndani yake ni kama vile lighting system ama taa kama vile upo ndani ya mji wa Las Vegas umeenda macasino ya hatari jinsi experience unayoipata ukiwa ndani ya club,” anasema Raheem.

“Pia sounding system, muziki ni wa kisasa, beat na vocal haviingiliani, screen za kutosha mle ndani, ukubwa umeongezwa, mashine ya cooling system ni ya hatari kiasi kwamba ukiwa ndani huwezi kusikia joto, hali ya hewa iko safi kabisa.”

Raheem anasema ratiba inaanzisha Alhamis ambayo ni siku ya madada ambapo kiingilio ni shilingi elfu 10 ambapo wasichana hupata coupon ya kinywaji kimoja bure.

Ijumaa na Jumamosi kiingilio ni shilingi elfu 15 ambapo theme yake ni ‘club bangers huku nyimbo kali zinazohit duniani zikichezwa.

Jumapili ni siku ya wasanii (Bongo Flava Night), wanafunzi na vijana ambapo hufanyika show mbalimbali za wasanii kwa kiingilio cha shilingi elfu 10.

“Kama unataka kuspend, kuparty, Bilz Night Club ndio sehemu pekee ambayo inabidi wewe ufike Posta mpya pale pale pa zamani,” ameongeza Raheem.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents