Burudani

Clouds TV yajikuta kwenye kitimoto kwa kurusha kipindi kuhusu ushoga, Makonda awatetea

Clouds TV ipo kwenye kitimoto baada ya kipindi chake cha Take One kinachoendeshwa na Zamaradi Mketema kumhoji shoga maarufu jijini Dar es Salaam.

13525591_1561679040794613_1803811388_n

Pamoja na Zamaradi kudai kuwa na nia njema ya kumhoji mtu huyo kwa madai suala hilo limekuwa tatizo nchini na ni muda wa kulizungumzia bila kificho, Watanzania wengi wameonesha kupinga kwa madai kuwa kipindi hicho kimetumika kulitangaza zaidi tatizo hilo.

Wapo pia wanaomtetea Zamaradi na hivyo kusababisha kuwepo na mgawanyiko mkubwa wa kimsimamo kuhusiana na suala hilo kama Tanzania imefikia hatua ya kuwepo mijadala ya aina hiyo kwenye runinga za taifa, seuze kuwahoji kabisa watu hao.

Hata hivyo Jumatano hii Clouds TV imelazimika kufanya kile kinachojulikana kama ‘damage control’ kujaribu kufafanua kwa wananchi kwanini ilikuwa sawa kuwa na kipindi cha aina hiyo.

“Suala hili ukilitazama positively utapata kujifunza mengi sana, hiki ni kipindi cha toba na kuhamasishana mema na kuacha mabaya, hili ni baya na lazima tulipinge na kulikemea na tusiwaangalie mashoga pekee tuwaangalie pia wale wanaoshirikiana nao ambao tuko nao ndani ya jamii,” alisema Zamaradi kwenye kipindi cha 360 cha kituo hicho alipohojiwa kueleza kwanini aliamua kufanya mahojiano na mtu huyo.

“Tusisubiri mambo yaharibike zaidi ndio tuanze kuzungumza lazima tuchukuwe hatua sasa, kama tunavyoweza kumhoji mwathirika wa madawa ya kulevya na kuamini kwa kujua njia alizopitia tutaweza kuepuka na kuwaelimisha ndugu na jamaa zetu ndivyo hivyo tujifunze walipokosea hawa,” alisisitiza.

“Je kuna tamthilia ngapi za nje zinaonekana kwenye runinga zetu zenye maudhui yenye hulka kama hizi na utofauti wa kipindi nilichofanya na tamthilia za nje ni kwamba kipindi changu kimelenga kukemea na kufundisha,kikubwa shtuka na chukua hatua. Leo ukienda kwenye kumbi za starehe kwenye taarabu haya yamekuwa ni mambo ya kawaida na pia ukipita Instagram utakuta page zao kabisa.”

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipiga simu kwenye 360 na kutetea kurushwa kwa kipindi hicho.

“Hatuwezi kubadilika kwa kuendelea kuishi katika mazingira tuliyoyazoea, tunakaa kwenye mazingira kama vile tupo sawa na akija wa kutuambia hatupo sawa tunawakebehi na kuwashambulia,” alisema Makonda.

“Tuamke na hizi hasira tuelekeze kwenye tatizo ambalo lipo kwenye jamii yetu, wazazi na walezi tujenge tabia ya kukagua watoto wetu tukiamka pia majirani zetu. Sisi kama Serikali tumeamshwa na pia inabidi waanze kutaja wateja wao ili jamii iwafahamu kwani inawezekana wateja wao wengine ni viongozi wa serikali,” aliongeza.

Hata hivyo bado wananchi wengi wameendelea kusisitiza kuwa kipindi hicho kimekiuka misingi ya utangazaji na kuitaka TCRA ichukue hatua.

Hizi ni baadhi ya barua zilizotukwa kwenye mamlaka hiyo ya mawasiliano kulalamikia kipindi hicho.

CmG2O0_WIAAZ8Yd

CmGnafBWEAA8wxz

CmGV61kWQAAIi4C

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents