Habari

Clouds Media International yafungua ofisi Jamaica

Clouds media International yenye makao yake makuu Abu Dhabi, imefungua ofisi mpya huko Kingston Jamaica zitakazohudumia ukanda wa Caribbean na kufungua fursa za kibiashara kwa kampuni tanzu za Clouds Media.

kusaga

Ufunguzi wa ofisi mpya nchini Jamaica unakuja ikiwa hata mwaka mmoja haujapita toka Clouds Media International ilipofungua ofisi zake Abu Dhabi.

Mkurugenzi mtendaji wa Clouds Media, Joseph Kusaga amesema ufunguzi huu ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu kuiwezesha kampuni yake kujitanua kimataifa ikiwa ni pamoja na uzalishaji na usambazaji vipindi, utoaji wa huduma za ziada kupitia simu za mkononi, masoko na usimamizi wa matamasha bila kusahau matumizi ya solar na vyombo vya habari.

“Jamaica na Caribia kwa ujumla ni soko jipya kwetu na kama Clouds mara zote huwa tunafikiria ni kwa namna gani tunaweza kujipenyeza katika masoko mapya ili kujitanua na kufanya biashara endelevu hivyo tunaona hii ni sehemu ya muafaka wa bidhaa na huduma tunazotoa” – Joseph Kusaga.

Shughuli zote za Clouds International zitasimamiwa na Dean Mundy, mtayarishaji wa muziki wa reggae na mfanyabiashara mzawa wa Jamaica mwenye uzoefu katika ukanda huo ambapo kukamilika kwa uzinduzi wa ofisi hizi kunadhihirisha umakini wa Clouds kujitanua kimataifa.

“Ni zaidi ya muongo mmoja sasa toka nilipokutana na Joe na wenzake nilipokuja Dar es salaam kwenye tamasha la Fiesta na haikunichukua muda kutambua kuwa hii ni kampuni ambayo tunaweza kufanya nayo kitu, japo kwa hakika sikujua ni kivipi ila kwa sasa uhakika ninao na pia fursa zipo, tuko tayari kufanya vitu vikubwa hapa Jamaica” – Mundy

Pamoja na Clouds Media International, makampuni tanzu kama status communications, Primetime International na Ray’s Solar yatakua na makao yake Kingston, ambapo status communications itajihusisha na utoaji huduma za ziada kupitia simu za mkononi, Primetime International itasimamia uandaaji wa matamasha na usimamizi wa Wasanii huku Ray’s Solar ikitoa huduma za umeme wa mionzi ya jua.

Source: Millardayo.com

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents