Burudani

Cliff Mitindo awashirikisha Fid Q, Gosby na Wakazi kwenye nyimbo 3 tofauti

Rapper wa ‘Complicated’ Cliff Mitimbo amewashirikisha Fid Q, Gosby na Wakazi kwenye ngoma tatu tofauti.

Cliff Mitindo

Cliff amesema kama alivyojipanga kufanya video ya ‘Complicated’, ndivyo atakavyofanya kwenye collabo hizo.

“Unajua hali ya muziki kwa sasa ni nzuri sana, shows kibao, hali hii inamfanya kila msanii kukaza na kuzifanya kazi zao bora. Mimi video yangu ya ‘Complicated’ nime-shoot Nairobi na director Kelvin Bosco. Hii ni kutaka kupata kitu kizuri zaidi. Pia kwa sasa kuna kuna kolabo mbili tatu ambazo kwa sasa nazifanyia kazi. Nimeingia studio na Fid Q, nimeingia studio na Gosby, nimeingia studio na Wakazi na zitakuwa zina-drop nyimbo yangu, kolabo halafu video, ndio plan yangu. Kikubwa watarajie kumsikia Cliff Mitindo kila mara,” rapper huyo ameiambia Bongo5.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents