Burudani

City of Tshwane yapoteza tshs bilioni 8.9 kwa kufutwa kwa tamasha la TribeOne

Rand milioni 65 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 8.9 za Tanzania za manispaa ya City of Tshwane zimepotea kutokana na kufutwa kwa tamasha la TribeOne ambalo Nicki Minaj na wasanii wengine walikuwa watumbuize.

676x380

Gazeti la City Press limeripoti kuwa rand milioni 10 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 1.4 alizolipwa Nicki Minaj ambazo hazitarejeshwa (non-refundable) ni sehemu ya fedha hizo ilizopoteza manispaa hiyo iliyokuwa wadhamini wakuu wa tamasha lenyewe.

Awali manispaa hiyo iliddai kuwa imetumia rand milioni 40 kuandaa miundo mbinu ya uwanja ambapo tamasha hilo la siku tatu lilipangwa kufanyika. Kesi kati ya waandaji wa tamasha hilo na manispaa hiyo inatarajiwa kuanza kusikilizwa kwenye mahakama kuu ya Pretoria Jumatatu ijayo.

Jiji linataka kuwalazimisha waandaji kuendelea na tamasha hilo kwakuwa limedai lilikamilisha wajibu wake.
Waandaji wanadai kuwa jiji hilo lilishindwa kukamilisha baadhi ya mahitaji ya miundo mbinu.

Tamasha lingefanyika weekend ijayo.

Msemaji wa TribeOne, Derrick Kaufmann alithibisha kwa gazeti hilo kuwa waandaji walipewa R25million na jiji hilo ili kuwalipa watumbuizaji. City Press limeripoti kuwa wasanii wengi walikuwa hawajalipwa fedha yao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents