Burudani

Cindy Rulz, Young Killer, Country Boy na Belle 9 waing’arisha video ya ‘Rock Star’ ya Young Dee

Rapper wa kike, Cindy Rulz, Young Killer, Country Boy na Belle 9 wanaonekana kwenye video ya wimbo mpya wa Young Dee, ‘Rock Star’. Video hiyo imeongozwa na Mkenya, Enos Olik huku wimbo huo ukitayarishwa kwa ushirikiano wa Maximilian, Erastone Machine, Moses Kinanda na Allan Mapigo.

https://www.youtube.com/watch?v=DNGjDNTIUm0

Cindy Rulz ambaye ni msichana pekee kwenye video hiyo, ameiambia Bongo5 kuwa haikumwia vigumu kufanya video na wanaumu tupu.

“Haikuwa ngumu na kwa ushirikiano wa kila mtu pale, walifanya kazi yangu iwe rahisi sana,” amesema. “MDB (Millian Dollar Boyz Entertainent) ni team nzuri iliyojipanga, hata Enos Olik na team yake pia. Ila lazima niseme being the only lady on set kulikuwa na privileges kidogo,” ameongeza.

“Utakuta wote wamesimama, lakini kunai le mpisheni Cindy akae jamani! Kila baada ya dakika kadhaa Young Dee anakuja anauliza like ‘do you need anything? Food, drink or anything?’ Au tu ‘uko poa’ Unazijua zile! Wakati Country wanatulia tu. Kama wanahitaji kitu ndio waseme, vitu kama hivyo.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents