Bongo Movie

Chuchu Hans: Sifikirii kuja kuachana na Ray

By  | 

Mpenzi wa muigizaji wa filamu, Vincent Kigosi aka Ray, Chuchu Hans amekanusha uvumi kuwa amepigwa chini na Ray na kudai kuwa hategemei kama watakuja kuachana.

Ray akiwa na Chuchu Hans

Chuchu amekiambia kipindi cha Take One cha Clouds TV kuwa wameamua kubadilisha aina ya maisha yao kwa kutopiga picha hovyo na kuweka mitandaoni.

“Sifikirii hicho kitu kuachana na Ray kiukweli sifikirii na kila kitu kinaenda kwa riziki na kama riziki yangu itakuwa imeisha basi nitaikubali hali. Lakini sifikirii hicho kitu kabisa,” alisema Chuchu ambaye naye pia ni muigizaji wa filamu.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.