Burudani

Christian Bella kuzindua rasmi ‘Nani Kama Mama’ Aug 29, azungumzia mradi wa kurudia nyimbo ukiwemo ‘Ukimwona’ wa Diamond

Muimbaji mwenye sauti iliyomfanya apewe jina la utani ‘Mzee wa Masauti’, Christian Bella atafanya uzinduzi rasmi wa wimbo wake unaotamba kwa sasa, ‘Nani Kama Mama’ aliomshirikisha Ommy Dimpoz.

Bella ameiambia Bongo5 kuwa uzinduzi huo utafanyika August 29, Mzalendo Pub Millenium Towers jijini Dar es Salaam na atasindikizwa na wasanii mbalimbali wakiwemo Ommy Dimpoz, Banana Zorro, Matonya, Cassim Mganga, Dully Sykes pamoja na bendi yake ya Malaika.

Muimbaji huyo amesema kuwa show hiyo itakuwa ya live.

“Ni show fulani ya heshima sana, nimealika akina mama waje, watu wa aina zote, wanaume wasiache wake zao nyumbani, kaka beba girlfriend wako, ni show tutakayoimba heshima kwa mama, kwa mara ya kwanza tukiperform live na Ommy Dimpoz,” amesema Bella.

“Ntaimba kwa hasira sana siku hiyo, nimejipanga nikamue kwa hasira sana,” ameongeza.

Katika hatua nyingine Bella amesema ana mradi wa kurudia nyimbo zaidi ya 10 za wasanii wa Bongo Flava anazozipenda ukiwemo ‘Ukimwona’ wa Diamond, ‘Me and You’ wa Ommy Dimpoz na ‘I love you’ wa Cassim Mganga.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents