Burudani

Christian Bella anunua nyumba ya $40,000 nchini Kongo

Hitmaker wa ‘Nani Kama Mama’ Christian Bella amesema ana furaha kubwa baada ya kununua nyumba nyumbani kwao Kongo (DRC) yenye thamani ya dola 40,000 (zaidi ya shilingi milioni 66) ambapo amedai kuwa ni matunda yaliyotokana na wimbo ‘Nani Kama Mama’.

bellagg

Akizungumza na Bongo5 leo akiwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam, Bella amesema alienda kuweka heshima nyumbani kwanza.

“Nimetoka kununua mjengo. ‘Nani Kama Mama’ imenipa heshima nyumbani. Nimenunua mjengo mkubwa sana, una thamani kama dola 40,000, sisi ni wasema ukweli. Sasa hivi ndo ninashuka airport. Nimekataa kupiga picha kwa sababu kuna marekebisho na nimenunuA karibu na uwanja wa ndege,”
alisema Bella

Akielezea sababu ya kununua nyumba Kongo na sio Tanzania, Bella amesema:

“Tanzania nitanunua nyumba yangu ya pili hii ni nyumba yangu ya kwanza, lakini pia siwezi kuanza kununua Tanzania sio kwangu. Leo wakitufukuza wale ambao sio raia means nitarudi kwetu ina maana ninaenda kupanga. Lakini mimi ya pili nitanunua hapa kwa sababu na familia pia iko hapa. Unajua sasa hivi kuna matatizo ya nchi yanaweza kutokea raia hawaelewani kwahiyo kila mtu anachukua zake. Sasa mimi nitaonekana vipi Tanzania ni star halafu kwetu hakuna kitu, ina maana nitarudi kwenye kupanga eti!”

Pia Bella amesema kwa sasa anataka kwenda kupumzika nchini Sweden.

“Nataka mashabiki wangu wanivumilie kidogo niende Sweden nikapigwe na upepo kidogo, maana yake inabidi pia ni relax kwasababu nafanya kazi kubwa. Nitulie bila kazi kidogo, nikirudi nakuwa mpya na nitawaletea manyimbo mapya na kila kitu mpya.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents