Burudani

Chris Brown kuendelea kukaa jela hadi June baada ya kesi yake kuahirishwa jana

Mwimbaji wa R&B Chris Brown ambaye kesi yake ya kumpiga Rihanna ilitarajiwa kuanza kusikilizwa jana (April 23) huko Washington D.C , nchini Marekani ataendelea kukaa jela hadi mwezi wa sita (June) baada ya kesi hiyo kuahirishwa.

Chris+Brown+Chris+Brown+Arrives+Court+Hearing+Abbazbzo2Vol

Kwa mujibu wa TMZ, ombi la Chris Brown kuachiwa limekataliwa na jaji wa kesi hiyo hivyo muda wowote atarudishwa Los Angeles ili kuendelea kusubiri muda wa kesi hiyo huku akiwa nyuma ya nondo.

Brown mwenye miaka 24 alitupwa jela mwezi uliopita baada ya kufukuzwa rehab huko Malibu alipokuwa akipata matibabu ya kukabiliana na hasira, baada ya kukiuka masharti.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents