Burudani

Chris Brown azungumzia uhusiano wake na Karrueche na kuthibitisha kuwa wako pamoja na hawakuachana

Hivi karibuni Chris Brown na girlfriend wake Karrueche Tran waliripotiwa kuachana kwa muda kabla hawajarudiana tena, habari ambazo mara nyingi hua zinatolewa na vyanzo vya karibu na mastaa hao.

chris-brown-and-karrueche-tran

Breezy amepata nafasi ya kusafisha kila kitu na kuthibitisha kuwa yeye na Karrueche wako vizuri licha ya kuwa walikuwa tayari wamethibitisha kwa picha mbalimbali za pamoja ambazo huwa wanapost Instagram.

Mtangazaji Sway Calloway alifanya mahojiano na Breezy kupitia MTV News na kuzungumzia uhusiano wake na Karrueche na habari zilizokuwa zinaripotiwa kuwa waliachana.

“Unaposoma vitu kwenye vyombo vya habari utaona hiki kilitokea, kile kilitokea, lakini nawaacha waongee kwasababu mwisho wa siku hiyo ni kazi yao”. Alisema Chris

Breezy ambaye ameachia album yake ya ‘X’ wiki hii, ameendelea kusema kwa miaka ya nyuma alipokuwa akiandikwa vibaya alikuwa ana ‘react’ vibaya lakini kwa sasa mambo yamebadilika na amekua.

“You’ve gotta mature at some point and not give them that attention…when it comes to all the extra hoopla, that just gets lost in translation with me.”

Chris pia aliulizwa kuhusu tukio la hivi karibuni la mpenzi wake aliposhambuliwa na mashabiki wa Beyonce baada ya kufanya utani juu ya nywele za Blue Ivy kupitia kipindi cha 106 & Park cha BET, Chris alisema alifanya mazungumzo na mpenzi wake kuhusu swala hilo na kumshauri nini cha kufanya wakati mwingine atakapokutana na hali kama hiyo.

“We had a conversation about that, too, but she’s good,” Breezy said. “I know the comment on the prompter was kinda left field — I don’t know who wrote it up, or [why] it was done — but I told her, next time, because I know it’s your first time doing this, just look at it and say ‘Hey, hey I don’t know about this’”

“But that comes with show business. At the end of the day it has to be something left, or most of the time, negative. I felt it was unnecessary.”

Ingia hapa kutazama mahojiano hayo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents