Burudani

Chris Brown anatumia saa 6 kila siku kufanya kazi za jamii kama sehemu ya adhabu yake

Chris Brown amegeuza adhabu yake kufanya kazi za jamii aliyopewa na mahakama kama kazi ya kila siku katika kipindi cha wiki 6 zilizopita. Lengo lake ni kuhakikisha anamaliza adhabu hiyo ndani ya wiki chache zijazo.

0328-chris-brown-getty-4

Mtandao wa TMZ umedai kuwa tangu November 13, Chris amekuwa akifanya kazi hizo kwa saa 6, siku tano kwa wiki kumaliza masaa 1,000 aliyopewa na mahakama mwezi January.

Adhabu hiyo ambayo ni sehemu ya kesi yake ya kumpiga Rihanna inahitaji afanye kazi nzito na amekuwa akifanya kazi za kupaka rangi, kufagia, kuondoa takataka, kubeba vitu na kazi zingine.

Ijumaa iliyopita, Chris alipiga mzigo huo kwa saa 6 na kisha kupanda ndege kwenda Jacksonville, FL ambako usiku huo aliotumbuiza. Baada ya hapo alisafiri hadi Columbia, South Carolina kwenye show ya Jumamosi na kisha kwenda Birmingham, AL kwenye show ya Jumapili.

Baada ya hapo alichukua ndege binafsi kurejea L.A. na kuendelea na kazi za adhabu hiyo Jumatatu.

Pamoja na kazi hizo, Chris anadaiwa kutolalamika kitu. Vyanzo vimedai kuwa siku anapanda tena kizimbani anatarajia kuwa amemaliza masaa hayo ya kazi.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents