Burudani

Chris Brown adai Drake angekuwepo kwenye album yake mpya X kama ingekuwa haijakamilika

Chris Brown amedai aliamua kuachana na bifu na Drake kwakuwa hakutaka kuendelea na maisha ya uadui tena.

chris-brown-billboard

Hivi karibuni Drake na Chris walionekana pamoja studio na pia kurekodi skit wakati wa tuzo za ESPY.

Akiongea na MTV News, msanii huyo amedai kuwa kama angekuwa hajaikamilisha album yake, X itakayotoka Jumanne ijayo, kungekuwa na wimbo aliomshirikisha Drake. “Kama album yangu ingekuwa haijakamilika,ingeweza kutokea.. kufanya kazi kwenye muziki ni kitu ambacho tutaendelea kujaribu kufanya itokee,” alisema Chris kuelezea uwezekano wa collabo na Dreezy.

“Najua kitakuwa kitu kikubwa kwa mashabiki kama wakisikia wimbo, lakini ni lazima uwe wimbo sahihi. Kwetu sisi sote tulipokuwa studio, alikuwa akisema ‘Aw man, Nahitaji kuwa na studio kama hii,’ nilisema ‘unamaanisha nini?’ alijibu: ‘Mara zote nakuwa humo na producer wangu ama vyovyote na nipo humo peke yangu.’ Unaona, mzuka wangu upo tofauti kidogo. Napenda kuwa na party. Ni kama club kwenye studio yangu. Kuna kama wasichana 15 au 20 na wanangu kadhaa na vinywaji kadhaa. Kila mtu anakula bata. Na huwa napata mzuka na nguvu kutoka kwao. Labda kama nataka kuandika kitu serious, wimbo wa majonzi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents