Michezo

China yaunda sheria mpya ya usajili, klabu kusajili wachezaji 3 tu kutoka za nje ya China

Huwenda ule usajiri wa kufuru ukapungua au kuongezaka katika klabu za China. Sheria mpya iliyoanzishwa nchini humo imezitaka klabu zinazocheza Ligi Kuu ya Uchina kusajili wachezaji watutu tu kutoka nje ya nchi.

Tevez ni mmoja kati ya wachezaji waliosajiriwa kwa pesa nyingi

Hapo awali sheria ya ‘4+1’ ukiwaondoa watalii wanne wa uraia wowote wakiongeza mchezaji mmoja wa Asia katika kikosi cha mchezo.

Timu pia zitatarajiwa kuwataja wachezaji wa China wawili wenye chini ya umri wa miaka 23 katia kikosi chao, na mchezaji mmoja mwenye umri wa miaka 23 katika kikosi cha kwanza cha wachezaji 11 na shirikisho la soka la China.

Pia kuzingatia ada ya kuwasaini wachezaji kinyume cha sheria katika uhamisho wa hivi majuzi.

Kiungo wa kati wa Chelsea Oscar na John Mikel Obi wameihamia China mwezi huu, huku mshambuliaji wa Manchester United na Machester City Carlos Tevez, akiripotiwa kuwa mchezaji anayelipwa zaidi ulimwenguni alipojiunga na Shanghai Shenhua mwezi Disemba.

Shenhua ni klabu miongoni mwa klabu itakayo kabiliwa na sheria hiyo mpya, kwani klabu hiyo inawachezaji sita ambao si raia wa uchina katika kikosi chake.

Klabu hiyo inawachezaji kama vile Tevez, mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Demba Ba na mshambuliaji wa zamani wa Newcastle Obafemi Martins

Costa amehusishwa na uhamisho wake wa kwenda Tianjin Quanjian, aliyemsahihi kiungo wa kati Axel Witsel kwa mshahara wa zaidi ya pauni milioni 15 kwa mwaka, mwezi huu wa Januari.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents