Habari

Chiku Ketto kuja na ngoma ya reggae ‘Sauti Yangu’

Femcee wa Tanzania Chiku Ketto ameingia studio kudhihirisha kwanini ana dreads kichwani kwa kutengeneza ngoma ya reggae. Ngoma hiyo iitwayo Sauti Yangu inatarajiwa kutoka hivi karibuni.

Chiku

Akiongea na E-News, Chiku amesema lengo la kuimba wimbo kwa mtindo wa reggae ni kuonyesha utofauti katika kazi zake na pia huo ni ujio wake mwingine kwenye fani aipendayo baada ya kukaa kimya kirefu na kufanya mambo mengine ya kijamii.

“Nilikuwa najipanga upya kwa ajili ya kuja kivingine na sasa nimekuja kivingine kweli kweli,kila atakayesikia kibao hiki atakubali kuwa nimerudi kwenye fani,” alisisitiza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents