Burudani

Chidi Benz: Kabla sijatoka mtaani walikuwa hawanikubali kabisa

Rapper wa muziki wa Hip Hop, Rashidi Abdallah Makwiro aka Chidi Benz amedai kuwa watu wake wa mtaani walikuwa hawamkubali kama anaweza kuimba.

Chid Benz

Akizungumza na kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio Ijumaa hii, Chidi Benz alisema mwanzoni mtaani alikuwa hakubaliki.

“Mimi nimeanza muziki kwenye mazingira magumu sana yaani watu walikuwa wanabisha na wanakataa tu wanasema hakuna kitu nachoweza. Nilijaribu sana kuwaonyesha kuwa hiki kitu naweza lakini walikuwa wanapinga sababu wao walikuwa siyo watu wa kujichanganya kwenye maclub, lakini mimi huko nilikuwa nakubalika kwakuwa ndio nilikuwa naenda kufanya kazi zangu huko Billicanas, Vijana n.k. Lakini baada ya kupata nafasi ya kuuzunguka muziki na kupata tuzo kibao nikaanza kupata support yao,” alisema Chidi Benz.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents