Burudani

Chid Benz adaiwa kushilikiliwa na polisi kwa kumjeruhi girlfriend wake wa zamani

Msanii wa Hip Hop kutoka pande za Ilala, Chid Benz anadaiwa yupo mikononi mwa polisi katika kituo cha polisi Pangani, Ilala kwa madai ya kumshambulia na kumuumiza vibaya, Aisha Sued ambaye anadaiwa alikuwa mpenzi wake wa zamani.
Chid Beenz_full

Kwa mujibu wa U heard ya XXL ya Clouds FM, imedaiwa kuwa usiku wa pasaka mwanadada Aisha Sued ambaye ni mkazi wa Ilala karibu na Kituo cha basi msaada garage amedai alishambuliwa na Chidi Benz na kuumizwa vibaya mdomoni hadi kushonwa nyuzi 18. Chid Benz mpaka sasa anadaiwa kushikiliwa na polisi katika kituo cha Pangani Ilala baada ya kupelekwa mahakamani leo na kuamrishwa na jaji kurudishwa ndani baada ya mwanadada huyo kushindwa kuongea chochote kutokana na maumivu ya mdomoni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents