Burudani

Chibwa kufanya collabo na Elephant Man

Mkali wa dancehall wa Bongo, Chibwa amesema anajindaa kufanya collabo na msanii wa Jamaica, Elephant Man.

chibwa

Chibwa aliiambia 255 ya Clouds FM kuwa connection hiyo aliipata kupitia DJ maarufu wa nchini Poland.

“Connection nilipata kutoka kwa Dj mkubwa ambaye anafanya vizuri nchini Poland na Jamaica,” alisema Chibwa.

“Huyo Dj sasa hivi ana uraia wa huko Poland lakini ni Mtanzania. Mdogo wake nilisoma naye ndo alikuwa akimtumia ngoma zangu huko akawa anazikubali sana, ndio akaamua kunisaidia kwa kuniunganisha na producer wa Elephat Man,” ameongeza.

“Na mimi nikamuunganisha na meneja wangu ndio akawa anasimamia kila kitu hadi wakapata muafaka kuwa Elephant Man atalipwa kiasi fulani na mwanzo ilikuwa tufanye na producer wake lakini Elaphant akawa amependa beat za producer wa huku kwahiyo hiyo kazi tutafanya na producer kutoka huku Bongo.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents