Burudani

Chibwa amuongeza Hard Mad kwenye wimbo ujao

Mkali wa muziki wa Dancehall Bongo, Chibwa amesema wimbo aliofanya na Hard Mad ndiyo unaofuata.

10422134_812063695567669_5972704573303766519_n

Hivi karibuni Chibwa aliachia wimbo wake mpya aliomshirikisha msanii kutoka Jamaica, Elephant Man na kuahidi kuachia video ya wimbo huo baada ya miezi miwili au mitatu.

Akizungumza na Bongo5, Chibwa amesema ‘wimbo wangu unaofuata nitauachia niliofanya na Hard Mad’.

“Nimefanya kazi nyingi za kimataifa, lakini kazi inayopewa nafasi kubwa na uongozi wangu ni wimbo niliofanya na Hard Mad. Baada ya kuachia video ya wimbo wa Dancehall Digital nitaachia wimbo niliofanya na Hard Mad,” aliongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents