Chenge akutwa na balaa jingine

Chenge akutwa na balaa jingine
Jeshi la polisi jijini Dar es salaam linamshikilia aliyekuwa Waziri wa
Miundombinu Andrew Chenge kwa tuhuma za kusababisha ajali iliyopelekea
wanawake wawili kupoteza maisha papo hapo.


Kamanda wa kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova amesema kuwa tukio hilo limetokea mnamo tarehe 27/3 majira ya saa 10 kamili ya usiku katika barabara ya Haile Selassie karibu na shule ya msingi Oysterbay.

Kova amesema kuwa Chenge (61) wakatia alipokuwa akiendesha gari lenye namba T512 ACE Toyota Pick Up Hilux alikuwa akitokea njia panda inayoingia mtaa wa St. Peters uelekeo wa Morogoro Store ndipo alipogongana na Bajaji No. T736 AXE iliyokuwa ikitokea maeneo ya Morogoro store ambapo abiria wawili wanawake waliokuwamo ndani ya bajaji hiyo walifariki papo.

Kamanda Kova amesema kuwa Chenge anashikiliwa wakati jopo la watu 5 linaendesha uchunguzi kufuatia ajali hiyo huku dereva wa bajaj akiwa anatafutwa kutokana na kukimbia mara baada ya tukio, miili ya marehemu bado haijatambulika huku ikiwa imehifadhiwa katika hospital ya Mwananyamala ambapo wote wanakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20-28.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents