Burudani

Chemical atoa msimamo wake kuhusu kufanya video nje ya nchi

Rapa wa kike bongo, Chemical amedai kuwa haoni sababu ya kwenda kushoot video Afrika Kusini lakini kama ikitokea location zimeisha Bongo ataenda.

33C090B100000578-3569871-image-m-42_1462227265535-1

“Kama video ya ‘Kama Ipo Ipo Tu’ niende kushoot Afrika Kusini kwa nini,” amehoji.

“Labda wanahisi nje ndiyo pazuri zaidi. Kama ikitokea nina wimbo ninahitaji kushoot video na location za Bongo zimeisha nitaenda nje na mimi kushoot pia,” ameiambia Bongo5.

“Video ya ‘Sielewi’ mwanzoni wakati inatoka watu walijua imefanyika South wakati imefanyika Tanzania kabisa tena Kigamboni.”

Mpaka sasa Chemical ameachia video mbili pekee ikiwemo ya wimbo ‘Sielewi’ aliomshirikisha Soprano.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents