Michezo

Cheka adai ‘ukata’ huwafanya wachezaji wengi kuingia kwenye biashara ya unga

Bondia anayeshikilia mkanda wa dunia wa WBF, Francis Cheka amesema kukamatwa na dawa za kulevya kwa bondia mwenzake Mkwanda Matumla na unga ni matukio yanayofanywa na wana michezo wengi ili kujipatia kipato kikubwa kwa mara moja.

Francis Cheka mashine

Akiongea na Bongo5 jana mjini Morogoro, Cheka alisema sababu inayosababisha wachezaji kubeba madawa ni kipato kidogo

“Kwa wana michezo wa Tanzania kama hivyo mtu anataka kuwa na gari zuri anafanya kazi za michezo na hapati pesa za kununua gari kwahiyo inabidi afanye kitu kama hiyo kubeba mizigo ili apate pesa ya kununua nyumba, alisema Cheka.

“Mimi nimejisikia huzuni sana sikujisikia furaha nilijisikia ni kitu ambacho kimeweza kudhalilisha katika mchezo wa masumbwi Tanzania lakini hakuna jinsi tutafanyaje, wao walikuwa kwenye kazi yao wenyewe kama wanavyokuwa kwenye boxingi, ila ni kitu ambacho kimekuwa kinasikitisha sasa hivi umekuta ulimwengu mzima wanapiga vita madawa ya kulevya lakini ni changamoto kwa watu wengine kujifunza.”

Aliongeza, “maswala yapo katika serikali na wahusika wapo katika serikali, kwaiyo ni mkondo mrefu kuzuia madawa ya kulevya hata hivyo nchi nyingi duniani tajiri zinahusika na madawa ya kulevya.”

Mkwanda Matumla akiwa na mshambuliaji nyota wa zamani wa timu ya soka ya Simba na Taifa, Joseph Kaniki ‘Golota’ walikamatwa Agosti 31, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Bole, Addis Ababa wakiwa na unga wakati wakijiandaa kupanda ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia tayari kwa safari ya kuelekea Paris, Ufaransa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents