Burudani

Chege: ‘Wauwe’ ni video kali katika video zetu ambazo tumefanya…Inatarajiwa kutoka Jumatatu Ijayo (July 14)

Msanii wa muziki kutoka kwenye kundi la TMK Family, Chege Chigunda amezungumzia ujio wa video ya wimbo ‘Wauwe’ ambayo ameisifia kwa kudai ni kali zaidi ya video zote walizowahi kufanya.

HHH

Akizungumza na bongo5, Chege amesema Jumatatu (July 14) wataachia video hiyo ili kuwapa fursa Watanzania kuangalia vilivyomo.

“Video ni kali sana kweli, ni video kali katika video zetu ambazo tumefanya, stori ya Wauwe inatakiwa Watanzania wasubiri kuona tulicho kifanya, nyimbo tumeiita Wauwe na tumefanya video ambayo ni kali. Ingawa wabongo wamekuwa wagumu kuelewa wamekuwa hawathamini kitu ambacho kimefanyika ndani, wanataka ukafanye nje hata kama ni mbaya watanzania wanaamini kwamba ni nzuri. Kitu ambacho sisi hatukubaliani nacho, siyo kila video inayofanyika nje ndo kali, kwaiyo naweza nikasema Adam anafanya video kali pia” Alisema Chege.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents