Burudani

Chege kutoa video mbili kwa mpigo usiku wa mwaka mpya

Msanii kutoka TMK Wanaume Family Chege Chigunda anatarajia kuupokea mwaka mpya kwa kutoa video mbili kwa wakati mmoja. Video hizo ni za single yake mpya ‘Chapa Nyingine’ aliyoitoa hivi karibuni pamoja na single yake nyingine ya miondoko ya Reggae inayoitwa ‘Binadamu’.

Chege

Meneja wa TMK Wanaume Family Said Fella, ameiambia Bongo5 kuwa video ya ‘Chapa Nyingine’ imefanyika Tanzania chini ya director wa Visual Lab/Next Level Adam Juma, huku video ya Binadamu ikiwa imefanyika nchini Kenya chini ya Ogopa Video.

“Video zote mbili za Chegge zitatoka kwa mara moja ule usiku wa mkesha wa mwaka mpya, hii single yake ya sasa na Binadamu. Ile Binadamu ni Reggae…audio yake iliwahi kutoka kimakosa ndio maana huisikii hata Redioni so tunafocus zaidi kwenye video ” alimaliza Fella.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents