Burudani

Chege awakutanisha Ay, Chidi Benz, Mwana FA, Dogo Aslay, Afande Sele, Q Chillah na Mh.Temba katika filamu yake “My Life”

Msanii nyota wa muziki wa Bongo Flava mtoto wa Mama Saidi namzungumzia Chege Chigunda amesema, kwa sasa yupo mbioni kuandaa filamu yake “My Life” ambayo itakuwa tayari mpaka kufikia mwishoni mwa February mwakani. Filamu hiyo ambayo inazungumzia maisha yake toka mwanzo na changamoto zilizompata tangu akianza musiki mpaka alipo sasa.

Kwa sasa msanii Chege ni mmoja kati ya wasanii waliofanikiwa sana katika fani ya muziki, ameweka wazi uamuzi wa kuingia kwenye filamu ili kutanua wigo wake wa sanaa na kutokana na kumiliki vipaji vingi ambavyo bado ajavifanyia kazi kama alivyoamua kuonyesha kipaji chake katika filamu.

Tunamnukuu Chege alichosema “najiamini kuwa naweza kufanya kazi za filamu, haitakuwa mara ya kwanza kwani huko nyuma nilishirikishwa katika filamu kadhaa, na nina uhakika sikufanya vibaya kwa hiyo naamini nitafanya kazi bora”, alisema Chege, ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wa Mwanayumba.
Katika Filamu hiyo amepanga kuwashirikisha wasanii kama Mh. Temba, Q Chillah, Ay, Afande Sele, Chidi Benz, Dully Sykes, Mwana FA na Dogo Aslay.

Wakati huo huo bongo5.com ilipata wasaa wa kuongea na Afande Sele ili atueleze amepokeaje habari ya kushirikishwa katika filamu moja na Chege. Afande Sele alisema yeye na Chege hawazuliani na wameshafanya kazi nyingi sana pamoja na wote ni marasi kwa hiyo hakuna tatizo, “ninachosubiri ni taarifa rasmi kutoka kwa Chege tufanye vyetu” alisema Afande Sele.

Msanii Chege ameweka bayana lengo lake ya kuisaida jamii kwa kuanzisha kitengo kitakacho saidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu, kitu ambacho kimemsukuma kufungua kituo, kutokana na jamii kumkubali na ndiyo waliomfikisha hapo alipo basi na yeye anatoa shukurani kwa kusaidia jamii.

Hata hivyo Chege alisema amejipanga kuwa na vyazo vingi vya biashara na misaada kwa jamii kwa lengo la kuboresha uchumi, muda unazidi kuyoyoma lazima kuwepo na maandalizi ya maisha ya baadae ambapo siku zote natamani maisha yawe mazuri au ya wastani ili nije kuisaidia jamii.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents