Burudani

Chege awa mpole, akubali kulipa gharama za mahari za mke wa mtu aliyemzalisha

Juzi tuliandika habari kuhusiana na skendo ya msanii wa hit ya ‘Mkono Mmoja’ Chege Chigunda aka Mtoto wa Mama Said kumzalisha mke wa mtu ambapo akiongea na U Heard ya Clouds FM mume wa msichana huyo aliyejitaja kwa jina la Jose mkazi wa Kasulu mkoani Kigoma alisema mke wake aitwaye Salma amejifungua mtoto anayefanana kila kitu na Chege.

Jamaa huyo alisema angeanza safari yake ya kuja Dar es Salaam kumleta Salma na mwanae kwa Chege ambaye anasema ndiye baba yake mzazi huku akitishia kumfanyiaa kitu mbaya staa huyo.

Licha ya kukanusha kutomfahamu Salma, jana Chege ameamua kumjibu Jose na kukiri kumtandika mimba Salma:

“Mke wako ndio mwenye matatizo aliniambia kwamba hajaolewa nikajua nipo peke yangu,” alisema Chege. Nilipogundua kaolewa ndio maana nilimtelekeza na hiyo mimba nilikuwa naifahamu kwamba nimempiga mimba, kwahiyo kwa hilo swala naomba unisamehe kama gharama nyingine tumalizane.”

Imedaiwa kuwa Jose alikuwa ameshaanza safari ya kuja Dar kwa Chege lakini jana aliishia Mbezi baada ya Chege kumuomba asije kwasababu angemharibia mambo yake na hivyo kusema atam atamrudishia nauli yake.

Kufuatia issue hiyo Chege aliongea na jamaa huyo amrudishieh ela ya mahari lakini amepewa shilingi laki nane tu huku yeye alitoa zaidi ya shilingi milioni moja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents