Burudani

Chege auzungumzia wimbo wake mpya ‘Wauwe’ na sababu ya kuendelea kufanya kazi na Adam Juma

Msanii wa muziki kutoka pande za TMK, Chege Chigunda amesema kuwa ameshamaliza kurekodi wimbo wake mpya uitwao ‘Wauwe’ na yupo kwenye mchakato wa kuanza kushoot video yake na director mkongwe Adam Juma.
Chege
Chege

Chege ameiambia Bongo5 kuwa anaamini kuwa Adam Juma atafanya mambo makubwa katika kazi hiyo itakayotoka baada tu ya kumalizika.

“Kwanza wimbo wangu umefanywa na maprodyuza wawili,Sheddy lever na Marco Chali, kwahiyo audio iko tayari natarajia kushoot video weekend ijayo na Adam Juma halafu itatoka. Mimi nafanya video zangu na Adam Juma because I believe Adam Juma na nitaendelea kufanya na Adam Juma mpaka nione mwisho wake. Kufanya nje ya nchi siyo solution ya kufanya kitu kizuri,kufanya kitu kizuri anaweza akafanya mtu yoyote na kama ingekuwa kufanya kitu kizuri ni nje basi wasanii wa ndani tusingefanya kitu. Kwahiyo mimi nitaendelea kufanya naye mpaka mwisho wake nione kitakuwa nini.”

Chege amedai kuwa ‘Wauwe’ ni ngoma ya party.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents