BurudaniVideos

Chege ampa shavu director wa ‘Mwendo tu’ ya Songa kushoot video ya ‘Kelele za Chura’

Chege hana mpango wa kwenda SA kushuti video ya wimbo wake mpya, Kelele za Chura aliomshirikisha Nandy.

Badala yake, muimbaji huyo ameamua kumpa shavu, Destro wa kampuni ya Wanene Entertainment kufanya video hiyo.

“Video inatoka baada ya wiki mbili na naishuti hapa hapa nyumbani, nashuti na kampuni ya Wanene Studios. Na director ambaye anashuti ngoma hii amewahi kufanya video moja tu lakini mimi nimeamini kwa kuiona hiyo moja tu, na watu wote najua watamuamini,” Chege amekiambia kipindi cha Street Joints cha Dizzim Online.

Staa huyo amesema licha ya wakati mwingine kwenda Afrika Kusini kufanya kazi zake, bado anaamini uwezo wa waongozaji wa video wa Bongo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents