Burudani

Chege amefunguka kuhusu albamu yake mpya

Msanii wa muziki Chege Chigunda amefunguka kuhusu ujio wa albamu yake ya tatu.

Muimbaji huyo amedai kuwa albamu hiyo ameipa jina la ‘Sweety Sweety’ na itakuwa na nyimbo 15.

“Albamu yangu itakuwa na nyimbo 15, itaitwa ‘Sweety Sweety’ na nimeshamaliza kurekodi nyimbo zote. Itatoka mwezi huu wa pili,” Chege amekiambia kipindi cha FNL cha EATV.

Msanii huyo ameongeza kuwa baada ya kukaa muda mrefu bila ya kuachia kazi yake akiwa na Mh Temba, sasa anatarajia kuachia wimbo mpya na rafiki yake huyo wa karibu kwa kuwa huu ndio muda muafaka waliokuwa wakiusubiri.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents