Burudani

Chege adaiwa kuzaa na mke wa mtu, mume kumpelekea mwanae

Msanii wa hit ya ‘Mkono Mmoja’ Chege Chigunda aka Mtoto wa Mama Said ametupiwa shutuma kali kuwa amemzalisha mke wa mtu.

Akiongea na U Heard ya Clouds FM leo, mume huyo aliyejitaja kwa jina la Jose mkazi wa Kasulu mkoani Kigoma amesema mke wake aitwaye Salma amejifungua mtoto anayefanana kila kitu na Chege.

Akizungumza kwa jazba, Jose amesema yuko tayari kwenda kuchukua vipimo vya DNA na kama vikionekana negative atamlipa Chege shilingi milioni tano.

Amesema kesho anaanza safari yake ya kuja Dar es Salaam kumleta Salma na mwanae kwa Chege ambaye anasema ndiye baba yake mzazi huku akitishia kumfanyiaa kitu mbaya staa huyo.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Chege aliyekuwa akiongea kwa dharau amesema hajui lolot na wala hamfahamu Salma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents