Burudani

Chance The Rapper atangaza kuja na ziara yake

By  | 

Baada ya kufanikiwa kuibuka kwa kishindo na tuzo tatu za Grammy zilizotolewa Jumapili iliyopita jijini Los Angeles, Marekani, Chance The Rapper ametangaza kuja na ziara yake ya show ya ‘Spring Tour’ itakayoanza mwezi April mwaka huu.

Ziara ya kwanza ya Spring inatarajiwa kuanzia San Diego April 24 na kumalizika Oktoba 3 katika mji wa Los Angeles.

Rapper huyo kutoka mji wa Chicago anatarajiwa kufanya ziara hiyo katika miji kadhaa ya Marekani ikiwemo Houston, Detroit, Cleveland, Toronto, Montreal, Washington DC, New York, Los Angeles na mingine.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments