Burudani

Chameleone hakuwa kikwazo kwenye video ya wimbo ‘Nakutunza’ – Barnaba

Msanii na mtayarishaji wa muziki wa High Table Sound, Barnaba, amekanusha tetesi za kwamba Jose Chameleone ndiye aliyesababisha kutokamika kwa video ya kolabo yao ya wimbo ‘Nakutunza’.
chameleone and Barnaba

Awali zilizagaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Jose Chameleone ndiye aliyesababisha project hiyo kutokamilika kutokana na kutoonyesha ushirikiano kwa Barnaba.

Akizungumza na Bongo5 hivi karibuni, Barnaba alikanusha uvumi huo huku akiwataka mashabiki wake kupuuza uvumi huo ambao unaweza kuharibu mahusiano yake na Chameleone.

“Chameleone ni broo wangu, sina tatizo naye na hizo habari siyo za kweli,” alisema Barnaba.

Barnaba amewataka mashabiki wa muziki wake kusubiria kazi pamoja video za kutosha kutoka High Table Sound.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents