Habari

CEO wa Apple Tim Cook atangaza kuwa ni shoga

Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya Apple Tim Cook ametangaza kuwa ni shoga na kwamba anajivunia kuwa hivyo.

m
CEO wa kampuni ya Apple, Tin Cook

Cook alitoa tamko hilo ili kujaribu kuwasaidia watu wanaong’ang’ana kutangaza jinsia zao katika ripoti iliochapishwa katika gazeti la biashara la kila wiki la Bloomberg. Wiki hii Cook alitoa changamoto kwa jimbo lake la Alabama kuhakikisha kuwa haki za mashoga na wale wanaobadili jinsia zinaheshimiwa.

“Mimi sijitambui kama mwanaharakati,lakini nimegundua nilivyofaidika na mikakati iliowekwa na wengine”,alisema Cook.

“Kwa hivyo iwapo watu wakisikia kwamba mimi ni shoga kutawasaidia baadhi yao ,ama kumpa faraja yule anayejisikia mpweke ama kuwashinikiza wengine kupigania haki zao,basi afadhali kutangaza maisha yangu ya faragha,”aliongezea.

Cook amesema amekuwa wazi kuhusu hali yake na watu wengi wakiwemo wafanyakazi wenzake katika kampuni ya Apple,lakini hilo halikuwa chaguo rahisi kutangaza hadharani kuhusu hilo.

Source:BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents