Habari

CECAFA Challenge Cup: Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes kwenda nusu fainali!!


Leo ni moja kati ya siku ambazo zitaingia katika kumbukumbu za Watanzania wengi wapenda soka, baada ya timu za Tanzania zinazoshiriki mashindano ya CECAFA Tusker Challenge Cup, Kilimanjaro stars na Zanzibar Heroes kufuzu kuingia robo fainali ya michuano hiyo.

Walikuwa ni Kilimanjaro Stars ambao walitangulia kuwapa Watanzania raha mara baada ya kuifunga timu ya taifa ya Rwanda Amavubi kwa mabao 2-0 baada ya wachezaji Amri Kiemba na John Bocco kufunga magoli yaliyoivusha timu hiyo.

Baada ya hapo ilikuwa ni zamu ya Zanzibar Heroes ambayo yenyewe imeweza kuingia pia nusu fainali kwa kuitoa timu machachali ya Burundi katika mchezo ambao ilibidi uamuliwe kwa njia ya matuta (penati) ambapo alikuwa ni kipa Mwadini Ally ambaye anaichezea timu ya Azam aliyeibuka shujaa baada ya kupangua penati 1 kati ya 6 zilizopigwa kuelekea kwake, hivyo kuifanya Zanzibar Heroes kuibuka washindi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents