Burudani

Cassper Nyovest akanusha kuwa alizomewa jukwaani kwa kuimba diss track ya AKA

Rapper wa Afrika Kusini, Cassper Nyovest amejibu juu ya uvumi ulioenea kuwa alizomewa jukwaani weekend iliyopita alipoimba diss track ya AKA kwenye show iliyofanyika Johannesburg.

nyovest

Baadhi ya mashabiki waliohudhuria show hiyo ‘Homecoming Picnic’ walidai kuwa umati ulimgeuka Cassper baada ya kutumbuiza ‘Dust2Dust’ ambayo ni diss track ya AKA, na wengine kusema kuwa baadhi ya watu walianza kuimba wimbo wa AKA, ‘Composure’ baada ya Nyovest kushuka jukwaani.

Cassper alikanusha taarifa hizo kupitia mitandao ya kijamii, na kuandika kuwa mashabiki walihitaji atumbuize kwa muda mrefu hivyo walichukia alipowapa nyimbo mbili na kushuka.

“Last night I supprised fans at #HCP with 2 songs and they were unhappy cause I got them excited and left when they wanted more. Now people are trying to twist the story and say fans booed me off stage. Don’t know why yall keep believing these lies but here’s a video of me walking off stage, do yor hear a single boo? STOP THE LIES!!!!”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents