Michezo

CAF yamteua Rais wa zamani wa TFF, Leodegar Tenga kuwania nafasi FIFA

Kamati ya Utendaji ya CAF, imemteua Rais wa zamani wa TFF, Leodegar Chilla Tenga kuwania nafasi ya uwakilishi katika Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Katika nafasi hiyo kutoka nchi za Afrika zinazozungumza Kiingereza, Tenga atachuana na Rais wa zamani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Zambia, Kalusha Bwalya na Kwesi Nyantakyi wa Ghana.

Wengine waliopitishwa kuwania nafasi ya uwakilishi katika Kamati ya Utendaji ya FIFA kutoka nchi za Afrika ni Tarek Bouchamaoui wa Tunisia ambaye anaingia kwenye kundi la nchi zinazozungumza lugha za Kiarabu, Kireno na Kihispaniola.

Kwa nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa wamo Constant Omari Selemani wa DR Congo na Augustin Sidy Diallo wa Cote d’Ivoire wakati nafasi nyingine za wazi ihuhusisha mwanamke mmoja, wamo Almamy Kabele Camara (Guinea), Chabur Goc (South Sudan), Danny Jordaan (Afrika Kusini), Hani Abo Rida (Misri) na Lydia Nsekera (Burundi).

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents