Burudani

Producer C9 ajipanga kurejea kutengeneza muziki wa hip hop

Mtayarishaji muziki wa Bongo Flava, C9 amesema mwaka huu ameamua kurejea kwa kasi katika kutayarisha ngoma za Hip Hop.

c9kanjenje2

C9 amedai kuwa tayari amekwishaanza kufanya kazi studio na wasanii wakubwa akiwemo Young Dee.

Mtayarishaji huyo pia, aligusia suala la kipato ambacho kimekuwa ni kidogo kwa upande wa muziki wa kizazi kipya na hii ikiwa ni moja ya sababu ya yeye kuuweka pembeni kwa muda.

“Mwaka huu nataka hasa niabadilishe muziki, mwanzo nilianza na muziki wa mduara, taarab,muziki wa bendi hiyo yote nimeshafanya ilikuwa bado muziki mmoja tu wa Hip Hop,” aliiambia E-News ya EATV.

“Nimeshaaanza kuongea tayari na wasanii wa Hip Hop na nimeshafanya kazi tayari na Young Dee,” aliongeza.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents