Burudani

Bushoke kuvunja ukimya kwa single mpya ‘Bwagamoyo’ na album

Hitmaker wa nyimbo kama Barua,Mume Bwege na Dunia Njia, Ruta Bushoke ambaye kwa sasa anaishi nchini Afrika Kusini, anatarajia kuachia wimbo mpya na album.

Ruta Bushoke

Bushoke ambaye anaishi jijini Pretoria, ameiambia Bongo5 kuwa kwenye album hiyo amemshirikisha baba yake Mzee Max Bushoke aliyewahi kuwa mwanamuziki wa bendi ya Sikinde huku kwa sasa akifanya kazi ya utangazaji nchini humo.

“Album yangu mpya ambayo nimemshirikisha Baba Mzee Max Bushoke inaitwa Bushoke international Album,” amesema Bushoke.

“Nimemshirikisha katika nyimbo kama 3. Bado haijaisha. Ila nyimbo kama 8 zipo tayari Ukiacha ‘She Want It’ niliyofanya na Face off kutoka Uganda. Kwa sasa “Bwagamoyo” ndio nyimbo rasmi ntaitambulisha nimeimba peke yangu. Nimefanya katika studio inaitwa Tidy Production Cape Town, producer ni Danro. Na pia nimeshafanya video za ngoma kama tatu pamoja na hii ya Bwagamoyo.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents