Burudani

Bruno Mars amkumbuka mama yake kwenye muziki wake

Bruno Mars amefunguka jinsi anavyomkumbuka mama yake Bernadette San Pedro Bayot aliyefariki Juni 1, 2013 katika muziki wake.

Hitmaker huyo wa 24K Magic, ameliambia jarida la Latina, Mama yake alikuwa ni muhimu zaidi katika maisha yake na kama angekuwa na uwezo angemfanya arudi tena duniani.

“Maisha yangu yamebadilika. Yeye ni zaidi ya muziki wangu. Ningefanya biashara muziki, ningemrudisha. Siku zote nilimsikia akisema, endelea kwenda na endelea kufanya hivyo,” amesema Bruno.

“Wewe unaweza kujua kwamba yupo na mimi kila niendapo. Ni kitu ambacho huwezi kufikiria – maumivu na mambo ambayo wewe unaweza kuyarudia: ‘Natamani, napenda tumefanya hii au kusema haya.’ Unaweza kuona maisha tofauti. Inaonyesha umuhimu halisi wa maisha. Hakuna kingine cha ziada katika hii dunia lakini familia na wapendwa wako,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents