Burudani

Sitti Mtemvu ajivua taji la Miss Tanzania 2014

Sitti Mtemvu amejivua taji la Miss Tanzania 2014.

Miss-Tanzania-Sitti

Hatua hiyo imetagazwa Jumamosi hii na Mkurugenzi wa Lino International Agency Limited, Hashim Lundenga kwenye mkutano na waandishi wa habari. Lundenga amesema Mtemvu aliitumia barua kamati ya Miss Tanzania kuhusiana na uamuzi huo.

“Kwa hiari yangu tena bila kushawishiwa na mtu na kwa kulinda heshima yangu na familia yangu natamka rasmi kuvua taji la urembo la Miss Tanzania 2014,” aliandika Sitti kwenye barua hiyo.

Lundenga akikana jambo
Hashim Lundenga akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari

Lundenga amesema taji hilo sasa litachukuliwa na aliyekuwa mshindi wa pili, Lilian Kamazima.

IMG_7423
Lilian Kamanzima (kushoto) atakuwa Miss Tanzania 2014, baada ya Sitti kujivua taji hilo

Miss Tanzania 2014 Lilian
Miss Tanzania 2014, Lilian Kamanzima

Vielelezo zaidi ya vitatu vilionesha kuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu alidanganya umri wake wa kuzaliwa. Vielelezo hivyo vilionesha kuwa mrembo huyo ana umri wa miaka 25, na sio 23 kama cheti chake ambacho kinaaminika kughushiwa kisemavyo. Passport yake, leseni ya udereva na taarifa za website rasmi ya ‘Idara ya Usalama wa ndani ya Marekani (Department of Homeland Security), pamoja na profile yake kwenye mtandao wa exproletalent.com vinaonesha kuwa alizaliwa May 31, 1989 na sio May 31 1991.

Sitti 2
Passport ya Sitti Mtemvu

Sitti alilazimika kupunguza miaka yake ili kwendana na sharti la mashindano ya Miss Tanzania yanayotaka mshiriki awe na miaka kuanzia 18 hadi 24. Hivyo kutokana na vielelezo hivyo, Sitti Mtemvu ana asilimia 100 za kuvuliwa taji na kupewa mshindi wa pili.

Passport
Leseni ya udereva ya Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu

Dalili za kuwepo udanganyifu huo, zilizoongezeka zaidi pale Mtemvu alipokutana na waandishi wa habari ambapo pamoja na kuwashutumu kwa kuandika habari za uongo, maelezo yake yalikuwa na walakini.

Sitti Mtemvu
Maelezo ya I-94 hupatikana kwa mtu yeyote kupitia website ya Department of Homeland Security. Kama unahitaji kupata taarifa ya safari za mtu nchini Marekani, andika majina yake, tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa, nchi alipopata passport yake na namba yake ya passport, utapewa taarifa hiyo

“Ukweli ni kwamba nina miaka 23 na cheti hicho hapo kinajielezea, mkitaka mnaweza kwenda hizo sehemu wanazotoa vyeti mkawauliza,” alisema Sitti. Mtemvu alisema cheti chake cha zamani cha kuzaliwa kilipotea akidai kuwa ni kutokana na maisha yake ya kusafiri mara kwa mara

“Kwahiyo ilibidi pale walipohitaji cheti nilete kingine,” alijitetea. “Sikutegemea hayo maswali leo kwahiyo sikuja nimejiandaa kihivyo,” alijibu mrembo huyo baada ya waandishi wa habari kumtaka awape ripoti yoyote ya polisi kuhusiana na kupotea kwa cheti chake cha mwanzo.

22
Taarifa za Sitti Mtemvu kwenye exproletalent.com zinaonesha kuwa ana umri wa miaka 25

Cheti cha kuzaliwa alichonacho sasa kinaonesha kuwa kilitolewa September 9 mwaka huu.

Sitti alitumia pia fursa hiyo kukanusha tetesi kuwa ana mtoto. “Sina mtoto, na mkitaka tunaweza kwenda hospitali sababu naona kama mmekuwa mkiniandama kwa vitu ambavyo si vya kweli,” alisema.
Akijibu swali la kuonekana kwa passport yake inayoonesha kuwa alizaliwa mwaka 1989 na huku kwenye cheti alichoonesha kikionesha amezaliwa May 31, 1991, Sitti alisema:

Sitogusia hilo suala kwasababu mimi nilivyokuwa nakuja kuomba ‘Umiss Tanzania’ niliombwa cheti cha kuzaliwa sasa hivyo vitu vingine ni personal life, kwahiyo sidhani hata nyie kama kuna mtu atakuja anachukua passport yetu, ama driving licence ya kweli au feki na kuiweka kwenye mtandao kama ni kitu ambacho mngependelea.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents