Breaking News

Breaking: Mbunge wa Chambani (CUF) Salim Hemed Khamis afariki dunia

By  | 

Mbunge wa Chambani (CUF),Salim Hemed Khamis amefariki dunia leo baada ya kulazwa jana kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili.

1700

Jana mbunge huyo alihudhuria vikao vya kamati za bunge lakini wakati akiendelea na kikao kwenye kamati alianguka ghafla kutokana na kujisikia vibaya na kupelekwa hospitali ya Muhimbili na wabunge wenzake.

Salim Hemed Khamis akibebwa na baadhi ya wabunge na watumishi wa Bunge baada ya kuanguka ghafla wakati akihudhuria vikao vya kamati za Bunge jana. (Picha: Mwananchi)

Salim Hemed Khamis akibebwa na baadhi ya wabunge na watumishi wa Bunge baada ya kuanguka ghafla wakati akihudhuria vikao vya kamati za Bunge jana. (Picha: Mwananchi)

Inadaiwa kuwa hali yake asubuhi ya leo iliendelea kuwa mbaya na majira ya saa sita na kitu mchana ikatolewa taarifa kuwa ameshafariki dunia. Sababu za kifo cha mbunge huyo inadaiwa kuwa ni shinikizo la damu.

Khamis aliyezaliwa September 20, 1951 amekuwa mbunge wa jimbo la Chambani tangu mwaka 2005.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments