Bongo5 Exclusives

Breaking: Kariakoo pachafuka, mabomu yanapigwa kila kona

Hii ni picha ya mtumiajia mmoja wa Facebook ambaye anadai imepigwa maeneo ya Msimbazi leo

Habari zilizotufikia hivi punde zinadai kuwa kuna hali mbaya katika maeneo ya Kariakoo jijini Dar e Salaam ambapo polisi wanapiga mabomu ya machozi kutawanya waislam wanaoandamana.

Kwa mujibu wa watu waliopo kwenye maeneo hayo maduka mengi yanafungwa na watu wanajifungia kwenye maduka hayo.

“Nipo maeneo ya kurasini, kuna helkopta ya polisi imepita katika anga hili muda huu. Sijui inaelekea wapi?” anasema shuhuda mmoja.

Naye mtangazaji wa Channel Ten, Salma Msangi ameandika kupitia Twitter, “Tanzania ya leo kama IRaQ, napita barabarani napishana na ma defender tu na mitutu, ndo twalindwa au wanalindaaa. Tanzania imeharibika tobaaaa, Waislam vs police.”

“Maandamano yameanza huku Mwananyamala….. Sauti za bunduki zinasikika!”

Tutaendelea kukupa updates kadri inavyowezekana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents