Michezo

Brazil, Argentina, Colombia na Paraguay wawasha moto katika mechi za kufuzu kombe la dunia 2018

Usiku wa Alhamisi hii zilichezwa mechi kadhaa katika bara la Amerika ya Kusini za kufuzu kucheza kombe la dunia mwakani nchini Urusi. Brazil wakiwa ugenini imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Uruguay.

Mabao ya Brazil yalifungwa na Paulinho aliyefunga mabao matatu pamoja na moja la Neymar, na goli lakufutia machozi la Uruguay lilifungwa na Edson Cavan kwa mkwaju wa penati. Katika michezo mingine James Rodrigues wa Real Madrid alifunga bao pekee kwa timu yake ya Colombia na kuisaidia kushinda kwa goli 1-0 dhidi ya Bolivia.

Nao Argentina wakiwa nyumbani walifanikiwa kushinda kwa bao 1-0 dhidi ya Chile. Goli la Argentina lilifungwa na Lionel Messi kwa njia ya penati. Paraguay wakawachapa Ecuador 2-1. Nao Venezuela wakatoshana nguvu na Peru kwa sare ya 2 – 2.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents