Habari

Boss Lady Zari wa Uganda akubali kuwa mke mwenza baada ya mumewe kuwa na mahusiano na mshiriki wa BBA ‘Amplified’ Sharon O!

By  | 

Boss lady Zari pamoja na mrembo Sharon O aliyekuwa mshiriki wa Uganda katika BBA Amplified ni warembo ambao wamejikuta katika mtafaruku wa mapenzi baada ya mioyo yao wote kumdondokea mfanyabiashara maarufu wa Uganda ambaye ameshindwa kuchagua upande mmoja kati yao.

ivan zari n sharon

Ilianza kwa drama nzito ya shutuma za kuibiana mume, baada ya Zari ambaye ameolewa na Ivan Ssemwanga na kufanikiwa kupata watoto watatu, alipomshutumu Sharon O kujihusisha kimapenzi na mume wake, kitendo kilicholeta vita ya maneno kupitia mitandao ya kijamii kati ya warembo hao.

boss lady3
Boss lady Zari

Vyanzo vya ndani vimeuambia mtandao wa Big Eye wa Uganda kuwa baada ya timbwili hilo kudumu kwa muda hatimaye beef hiyo imezikwa rasmi na kuleta sura mpya katika familia ya Ivan ambaye ni mfanyabiashara tajiri wa Uganda mwenye makazi yake Afrika Kusini.

Inasemekana baada ya Ivan na Zari kuachana kwa muda kutokana na mvutano kuhusu Sharon, hatimaye wameyamaliza baada ya kikao cha kifamilia kufanyika kikiwakutanisha Zari, mumewe Ivan pamoja na mama yake na Zari na wakayamaliza kwa maamuzi yafuatayo.

Sharon-O3
Sharon O

Zari amekubali kumaliza tofauti zake na Sharon aliyekuwa akimtuhumu kumuibia mume, lakini kubwa zaidi katika hili ni kuwa amemkubali Sharon kuwa mke mwenza kwa mumewe Ivan.

Katika mkutano huo uliofanyika wiki iliyopita, Zari alimuomba msamaha mumewe kwa yale yote aliyokuwa akifanya kwa lengo la kulinda penzi lake kwa mumewe dhidi ya Sharon na kisha kumpigia Sharon kumuomba msamaha pia.

Kufuatia kusamehewa na Ivan pia alimuamuru Zari kuifunga akaunti yake ya facebook ambayo alikuwa akiitumia kuandika shutuma hizo kitu ambacho alikifanya, (hata mimi nimejaribu kumtafuta facebook hapatikani).

Chanzo hicho kinaendelea kusema katika mkutano huo Zari alimkubali rasmi na kumtambua Sharon O kama mke mwenza lakini kwa masharti kwamba, amuheshimu kama mke mkubwa sababu yeye ndiye aliyetangulia kuolewa na Ivan ambaye walefanikiwa kupata watoto watatu na pia ahusishwe katika maamuzi yote makubwa ya familia.

Ivan
Ivan

Ivan pia aliahidi kuwa hakuna kitakachobadilika katika familia sababu kama pesa anayo hata ya kuhudumia wake 10.

Baada ya kuyamaliza hivi sasa Zari na Sharon O kwa kushirikiana wako katika maandalizi ya kumtambulisha Ivan rasmi kwa familia ya Sharon (mmmmh! Is Zari real on this?).

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments