Michezo

Bosi wa mashindano ya Langalanga Bernie Ecclestone apigwa chini

Bernie Ecclestone ambaye alikuwa mwenyekiti mtendaji wa mashindano ya Formula one (Langalanga) ameondolewa kwenye nafasi hiyo baada ya Shirika la habari la Liberty la Marekani kukamilisha mkataba wake wa dola bilioni 8 ya kuumiliki mchezo huo.

Nafasi ya Bernie (86) ambaye ameongoza mchezo huo kwa takribani miaka 40 imechukuliwa na Chase Carey ambaye alikuwa makamu mwenyekiti wa kampuni ya 21st Century Fox. Akiongea na Auto Motor und Sport Jumatatu hii, Ecclestone alisema, “forced out. I was dismissed. This is official. I no longer run the company. My position has been taken by Chase Carey.”

Wakati huo huo shirika hilo la Liberty limeongeza watendaji wengine ambao watasimamia mchezo huo akiwemo meneja wa zamani wa magari ya Mercedes, Ross Brawn na Mkurugenzi wa ufundi wa zamani wa Ferrari ambaye alikuwa akifanya kazi kwa niaba ya mshauri wa Liberty ambaye ameteuliwa kuongoza kazi za ufundi katika kampuni ya mashindano ya F1.

Naye afisa mkuu wa ESPN, Sean Bratches ameteuliwa kuhusika na maswala ya kibiashara.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents